Sunday, June 5, 2011

SHUKURANI KWA BABA NA MAMA

              Ni mila na utamaduni wa mtanzania kutoa shukurani za dhati kwa yeyote atakayemsaidia kwa njia moja ama nyingine.Basi na nikiwa mtanzania sina budi kutoa shukurani zangu za dhati kwa wazazi wangu si kwa kunizaa bali kwa tabu namisukosuko walioipata wakati toka utotoni mpaka hapa nilipofikia.Japokuwa nimoja ya majukumu yamzazi ila kwa upande wangu ilikuwa imezidi hasa katika kuniwezesha katika swala zima la elimu.
Kwa kiasi kikubwa wamekuwa nguzo,wanga na tekemeo la maisha yangu toka shule ya msingi hadi kidato cha sita sitakuwa nimekosea kusema wasinguwa wao nisingefika hapa nilipo niseme nawashukuru sana mama na baba kwa kazi kubwa mliofanya mungu awape maisha marefu na moyo wa upendo si kwa watoto wenu hata kwa ndugu jamaa na marafiki.
       Nikweli safari ya maisha yangu hasa ya shule ilikuwa chini ya mikono ya wazazi wangu ila kwa upande mwingine wapo ndugu na marafiki walichangia safari hii kufika hapa nilipo nao ni,walimu wote wa shule ya msingi MARETI  1994-2001 shukurani za dhati kwa mwalim NIPA ambaye alikuwa mwalimu wangu wa darasa la kwanza,walimu wote wa KIGONIGONI SECONDARY SCHOOL 2002-2005,walimu wote wa KIRONGAYA SECONDARY 2006-2007,walimu wote COSTAL HIGH SCHOOL 2008-2010.Pia siwezi kumsahau MR. RAJUNI HASSANI MTETI ambae nimeishi nae kwa kipindi cha miaka minne nikiwa Kigongoni secondary,MR AND MRS BAKARI HUSSEIN MTETI nikiwa Kirongaya secondary,MARIAM SAWAYA MSANGI ,ADAM DIWANI BWANAHINDI NA HAMIMU MUSSA,nikiwa Costal high school na wengine wengi.kwa pamoja nawapenda sana mungu awe nanyi.
         Katika safari kama hii hapaachi kutokea furaha na karaha kwa yeyote nilie mkera basi namuombea kwa m/mungu apewe moyo wa huruma na upendo anisamehe.

2 comments:

  1. Nimekuona mzazi, pole kwa safari ndefu, uckate tamaa kwani kwanza ndo tumeingia katisa highway kuelekea huko yalipo maisha, ni heri kushukuru kwani kibongobongo, kushukuru ni kuomba tena, wapende wapende wakuchukiao na wachukize wakupendao ukiwa katika haki,

    "siku zote akosaye kwa kuvunja sheria na akakubali kutumikia kifungo sio kuwa analipia adhabu bali huonesha ni jinsi gani anavyo heshimu sheria"

    "Darkness can not drive out darkness, only light can do that,
    Hate can not drive out hate,
    only love can do that"

    Wewe sio rafiki yangu, na nitakuwa miongoni mwa maadui zako endapo utanifanya kuwa rafiki yako, sipendi na sitapenda uniite ivyo, ni kwa sababu tu wewe ni ndugu yangu,
    basi kama wewe ni ndugu yangu, basi wewe ni rafiki yangu mkubwa, ninakupenda, nakujali nakuheshimu na nakutakia maisha yenye afanikio, amani, hekima na upendo kwa wote.

    Kwa asili binadamu tu wasahaulifu, ila sidhani kuwa visima vya kale hufukiwa.

    Be bleased and stay cool brother.

    ReplyDelete
  2. KATIKA VITABU VIWILI VITAKATIFU TUNAVYO VYIAMINI KIMOJAWAPO KIMEANDIKWA YA KWAMBA ,HAMUZI KUISHI KWA KIPANDE CHA MKATE ILA HATA KWA NENO. NIMEYAKUBALI MANENO YAKO MKUU. MUNGU AKUWEKEE MKONO WA BARAKA AMIN

    ReplyDelete